Kampuni ya Ugiriki yakiri kufanya magendo ya mafuta ya Iran

Kampuni ya usafirishaji meli ya Ugiriki, imekubali makosa kwa  kusafirisha kwa magendo mafuta ghafi ya Iran ambayo yemewekewa vikwazo, na kukubali kulipa faini ya dola milioni 2.4, kwa mujibu wa nyaraka mpya za mahakama ya Marekani, ambazo shirika la habari la Associated Press imeziona.

Kesi ya sasa ya umma dhidi ya kampuni ya Empire Navigation, ambayo inakabiliwa na kipindi cha miaka mitatu cha uangalizi, ilikubali kuingia makubaliano, kufanya kuwa kukiri kwa kwanza kwa waendesha mashitaka wa Marekani kwamba Marekani ilishikilia mapipa milioni 1 ya mafuta kutoka meli ya mafuta ya Suez Rajan.

Kashfa hiyo inayohusiana na meli ilisababisha mivutano baina ya Washington na Iran, licha ya kwamba zinafanyia kazi biashara za mabilioni ya dola kutokana na mali za Iran zilizo shikiliwa Korea Kusini ili kuachiliwa kwa Mmarekani mwenye asili ya Iran, anaye shikiliwa mjini Tehran.