Kampuni ya simu kutoka Hong Kong limeamua kuingia kwenye soko la Afrika Mashariki. Kampuni hiyo kwa jina Zuri imebaini kuwa inashirikiana na ile ya Despec kuzindua simu za kisasa nchini Kenya, Tanzania na Uganda.
Zuri inasema kuwa itazindua simu aina nne kwenye soko hilo. Simu hizo ni C41, C46, C52 na S56. Mkurugenzi mkuu wa Zuri, Vikash Shah, amesema kuna nafasi kubwa ya ukuaji katika eneo la Afrika Mashariki ambapo matumizi ya simu za kisasa (smartphones) yanaendelea kuongezeka.
Simu ya C41 ina urefu wa inchi 4 yenye uwezo wa megabite 512 na inapatikana kwa rangi nyeusi na nyeupe. C46 ina urefu wa inchi 4.5 ikiwa na megabite 512 na kamera yenye uwezo wa Megapitzel 8. Simu ya C52 nayo ina urefu wa inchi 5 ikiwa na uwezo wa gigabite 1 na kamera ya megapitzel 8. Simu ilio kubwa kabisa ni ile ya S56 ilio na urefu wa inchi 5.5 na hyenye uwezo wa kuchuka sim card 2 kwa wakati mmoja na inayotumia mfumo wa Android 5.1 Lollipop.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni shirika ya Despec, Riyaza Jamal, amesema kuwa wana nia ya kuleta simu za kisasa kwenye soko la Afrika Mashariki ambazo ni tofauti na zingine zozote.
Anasema mikakati ya mauzo iliowekwa na Zuri, pamoja na ujumbe unaoenezwa bila kusahau ubora wa bidhaa zao kwa pamoja zitachochea mauzo makubwa kwenye eneo hilo la Afrika Mashariki.