Kampuni Sanergy yaboresha huduma za vyoo katika maeneo ya mabanda Nairobi

Mkazi mmoja mwa maeneo ya mabanda Kenya akitembea kuepuka uchafu katika maeneo ya ,mabanda ya Kibera nje kidogo ya jiji la Nairobi Juni 28,2002.

Kampuni moja ya Kenya ambayo inaboresha huduma za usafi wa vyoo katika maeneo ya mabanda mjini Nairobi na kugeuza uchafu huo kuwa ni mbolea kwa ajili ya wakulima.

Kampuni moja ya Kenya ambayo inaboresha huduma za usafi wa vyoo katika maeneo ya mabanda mjini Nairobi na kugeuza uchafu huo kuwa ni mbolea kwa ajili ya wakulima.

Anita Mutinda anakwenda kwenye kijumba kidogo kilichoko kwenye makazi yake ya muda ambayo anayaita numba, katikati ya Mukuru kwa Ruben, ujirani maskini katika mji mkuu wa Kenya.

Kijumba hicho ni moja ya vyoo ambavyo vimewekwa na kampuni ambayo inatoa huduma muhimiu katika eneo hilo. Ni moja ya sababu ambazo Anita amekodisha hapo na kuishi kwa takriban miaka mitano hivi sasa.

Anita anasema “maisha nilipokuwa nikiishi hapo kabla ilikuwa vigumu sana kwasababu, ilinilazimu nilipe shiling tano zinazohitajika kutumia choo cha umma, na. ilikuwa mbali na nyumbani. Hapa, sina haja ya kulipa hata senti moja kupata huduma ya choo.”

Mwenye nyumba wake, Deborah Kerubo, anasema upatikanaji wa huduma ya vyoo kwenye eneo lake limekuwa ndiyo kigezo kikuu cha kupata wapangaji.

“Wapangaji wanataka huduma hii wakati wote mchana na usiku. Kama haipo, wataamua kwenda kwingineo,” anasema Deborah na kuongeza “mpaka wapate kile wanachokitafuta.”

Mukuru kwa Ruben, kama yalivyo maeneo mengi ya mabanda katika mji mkuu wa Kenya, hakuna mfumo wa maji taka. Inakadiriwa kuwa asilimia 60 ya idadi ya watu wanaishi bila ya huduma za vyoo.

Elijah Gachoki, afisa afya katika kituo cha afya cha jamii kwenye eneo, anasema hali hizi ni sababu kubwa sana za magonjwa ya kuambukiza.

“Tulianza kwa kupata magonjwa yatokanayo na maj machafu, ugonjwa wa macho na magonjwa mengine ya ngozi, kwahiyo kuna haja ya huduma bora za usafi na zinazokidhi mahitaji,” amesema Gachoki.

Ni mwanya ambao unaelezewa na meneja uhusiano wa nje wa Sangery kampuni ambayo inatoa huduma za vyoo ambazo zinatenga maji na uchafu mwingine na kusaidia katika kusimamia jukumu usafi katika makazi yasiyo rasmi.

Sheila Kibuthu, meneja uhusiano wa nje wa Sanergy Kenya anasema kampuni yake inaamini haipotezi uchafu wowote.

“Katika hali ya kawaida, tunahakikisha kwamba tunatoa huduma za kusimamia kuzuia uchafu ambako kote kwenye uchafu wa vinyesi ambako unaondolewa kwa usalama zaidi na kusafirishwa kwenye sehemu maalum na kufanyiwa mchakato ili utumike tena,” anasema Kibuthu.

Uchafu wa vyoo unakusanywa kila siku na kuchangwa na uchafu mwingine kutoka kwenye jamii. Halafu unapitia mchakato maalum kwenye kiwanda cha Sanergy nje ya viunga vya Nairobi na kugeuzwa kuwa mbolea isiyo na kemikali na bidhaa nyingine za kilimo ambalo hutumika kwa malisho ya mifugo.

“Moja ya changamoto kubwa sana kwa wakulima hivi leo wanayokabiliana nayo ni ardhi yenye rutuba na kwa njia hiyo wakulima wanaweza kupata mavuno mazuri,” Kibuthu ameongezea.

Sanergy inaamini wakulima wengi zaidi watahudumiwa kama huu mzunguko wa kugeuza. Uchafu kuwa bidhaa yenye tija, utatoa huduma muhimu inayohitajika kwaa.

Hivi sasa kampuni ina zaidi ya vyoo 5,000 ambavyo viko kote katika maeneo yenye makazi yasiyo rasmi mjini Nairobi, wakihudumia zaidi ya wakazi 140,000.