Kampuni ya mitandao ya Meta Platforms yashtakiwa kwa kuchochea vita Ethiopia

Nembo ya Facebook

Kampuni ya  Meta Platforms (META.O) imeshtakiwa nchini Kenya Jumatano kwa kuruhusu machapisho ya manyanyaso na chuki kutoka Ethiopia kushamiri kwenye Facebook, na kuchochea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kesi hiyo iliwasilishwa na watafiti wawili raia wa Ethiopia na kundi la Kenya la kutetea haki la Katiba Institute, wakidai kwamba mifumo ya mapendekezo ya Facebook imeimekuzwa machapisho hayo nchini Ethiopia, ikiwemo mengine kadhaa yaliyotangulia kuhusu mauaji ya baba wa mmoja wa watafiti.

Kesi hiyo pia imesema Meta imeshindwa kutumia teknolojia ambayo itaweza kutambua machapisho hatari zaidi na kuajiri wafanyakazi kufuatilia maudhui kwa lugha ambazo zinatumiwa na vituo na matandao wake mjini Nairobi.

Msemaji wa Meta Erin McPike alisema hotuba za chuki na kuchochea ghasia vilikuwa kinyume cha kanuni za Facebook na Instagram.