Kampuni ya Huawei kutoka China inaonekana tishio kwa Marekani

kampuni ya mawasiliano ya Huawei kutoka China

Hii inanafuatia uchunguzi ulioripotiwa na idara ya ujasusi ya Uholanzi kwenye mtandao kwamba itaipatia kampuni ya Huawei fursa isiyo rasmi za takwimu za watumiaji

Marekani kwa mara nyingine inatoa wito kwa washirika wa ulaya kuchukuwa tahadhari kutokana na hatari ya usalama inayotokana na kampuni kubwa kabisa ya teknolojia na mawasiliano ya China ya Huawei wakati nchi zinajenga mitandao yao ya 5G.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alieleza Jumatatu baada ya mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi, Stef Blok huko The Hague kwamba wamekuwa wazi na ombi lao ni kwamba washirika wao na marafiki zao pamoja na familia zao wasifanye lolote ambalo litahatarisha maslahi yao wanayoshirikiana upande wa usalama au kudhibiti uwezo wao wa kushirikiana taarifa nyeti.

Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani

Matamshi hayo ya mwanadiplomasia huyo wa cheo cha juu Marekani yanafuatia uchunguzi ulioripotiwa na idara ya ujasusi ya Uholanzi kwenye mtandao kwamba itaipatia kampuni ya Huawei fursa isiyo rasmi za takwimu za watumiaji.

Pompeo na Blok walikutana pembeni ya mkutano wa siku tatu juu ya ujasiriamali duniani mwaka 2019-GES unaoongozwa na Marekani na Uholanzi huko The Hague.

Mkutano huo maarufu unaofanyika kila mwaka unawakutanisha wajasiriamali, wawekezaji pamoja na wafuasi wao kutoka zaidi ya nchi 120.