Kampuni ya Adani Energy Solutions ilisema Jumamosi kwamba Kenya kufuta mradi wa usambazaji umeme wa takriban dola milioni 736 ilikuwa hakuna haja ya kuelezea kanuni zozote kwa mujibu wa sheria ya kanuni za hisa za India kwa vile ilikuwa ndani ya mpango wa kawaida wa biashara.
Kampuni ilisema ilikuwa inajibu ombi la kutaka ufafanuzi kutoka Soko la Hisa la Bombay na Soko la Hisa la Taifa baada ya shirika la Habari la Reuters kuripoti kuwa Rais wa Kenya aliamuru kufutwa kwa mkataba wa miaka 30 wa ushirikiano wa umma na binafsi.
Katika kuongezea hilo kampuni hiyo inaeleza kuwa hakuna athari za kibiashara kwa ripoti ya vyombo vya habari juu ya shughuli za kampuni, taarifa ya Adani Energy Solutions ilisema.
Rais William Ruto pia alisema siku ya Alhamisi aliamuru kufutwa kwa mchakato wa usimamizi ambao ulikuwa unatarajiwa kutoa tuzo ya udhibiti wa uwanja mkuu wa ndege wa Kenya kwa kampuni ya India ya Adani Group.