Kampeni za uchaguzi Marekani zachukua mrengo mwingine

wagombea urais Mrepublican Donald Trump na Mdemocrat Hillary Clinton

Trump amekuwa akirudia mara kadhaa kwamba Clinton anatakiwa kuwa jela kutokana na matumizi yake ya barua pepe wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Mgombea urais kupitia chama cha republican Donald Trump ameshutumu vyombo vya habari kwa kuwa na ushawishi katika uchaguzi mkuu wa Novemba 8 na kuonesha upendeleo kwa mpinzani wake wa chama cha Democratic.

“ Hillary Clinton alitakiwa kushitakiwa, na alitakiwa awe jela “. Trump alisema hayo katika mtandao wa twitter Jumamosi asubuhi. Na badala yake anagombea kuwa rais wa kile kinachoonekana kama uchaguzi ulioibwa.”

Trump amekuwa akirudia mara kadhaa kwamba Clinton anatakiwa kuwa jela kutokana na matumizi yake ya barua pepe wakati alipokuwa waziri wa mambo ya nje.

Baada ya uchunguzi , mkurugenzi mkuu wa shirika la kijasusi-FBI, James Comey alitangaza mwezi Julai kwamba tuhuma dhidi ya Clinton hazikuwa na msingi.

Maelezo ya Trump ya hivi karibuni yamekuja siku moja baada ya wanawake wengine wawili kudai kuwa bilionea huyo muuzaji wa nyumba alitaka kufanya nao mapenzi kwa lazima.