Marekani yapata njia ya kutoa taarifa za simu za Apple

Joey Mink demonstrates outside the Apple store in New York protesting the FBI for obtaining a court order that requires Apple to make it easier to unlock an encrypted iPhone.

Hatimae Wizara ya Sheria ya Marekani imepata njia ya kutoa taarifa kwenye simu ya iPhone 5C iliotengenezwa na kampuni ya Apple kwa kutumia mbinu ambayo haijatolewa wa umaa.

Hatua hiyo imefikisha kikomo kesi iliokuwa ikiendelea kati ya Serikali na kampuni ya Apple kuhusiana na simu ya mshukiwa wa shambulizi la mwaka jana mjini San Bernardino, California.

Sasa swali lililobaki ni la viwango vya habari ambavyo Serikali inaweza kupata kutoka kwa raia wake na mbinu zinazotumika. Mjumbe wa baraza la Congress kutoka California, Darell Issa, ambae amekuwa akiongoza kampeni ya kulindwa kwa taarifa za kibinafsi, amesema ni bora kesi hiyo ilivyomalizika bila kuongoja uamuzi wa mahakama lakini swala la habari za kibinafsi lingali halijatatuliwa.