Katika ilani yake ya uchaguzi, chama cha Jubilee kimeeleza bayana kuwa kina mikakati madhubuti ya kupambana na ufisadi nchini Kenya. Suala hili litapewa kipaumbele katika serikali yao.
Wakati ambapo muungano wa upinzani wa NASA umeahidi kuwa hautastahmili vitendo vyovyote vya ufisadi na kuelezea kuwa nchi imeathiriwa na rushwa iliyokithiri hivyo basi endapo watafanikiwa kuingia mamlakani rushwa haitakuwa na rafiki katika serikali yao.
Licha ya ahadi hizi ambazo zimekuwa ni kama nyimbo katika mikutano yao ya kampeni,Wakenya bado wanakumbuka baadhi ya kadhia kuu za rushwa ambazo zimeikumba nchi hiyo na hivyo kutaka kuona kuwa hilo linatendeka kweli na siyo maneno matupu ya wakati wa kampeni.
Kenya mwaka jana ilikumbwa na kadhia tano kuu za rushwa mojawapo ikiwa ni ile iliyomuondoa mamlakani waziri wa ugatuzi, Anne Waiguru kufuatia upotevu wa fedha katika idara ya huduma ya vijana ya taifa ( NYS).
Nyingine ni ile ya Afya House ambapo uptoevu wa fedha katika wizara uliifanya serikali ya Marekani kusitisha msaada wa moja kwa moja kwa wizara hiyo ikielezea wasi wasi wake mkuu katika suala la ufisadi.
Taasisi ya evans kidero ambayo ilimhusisha Gavana wa Nairobi mwaka jana ambapo katika akaunti yake ya benki alikuwa na kiasi cha shilingi bilioni 2.7.
Lakini Kenya imeshakumbwa na kadhia nyingine kadhaa za rushwa katika miaka iliyopita ikiwemo ile ya Goldenberg ambayo ilizungumziwa sana katika uchaguzi uliopita.
Lakini vyama hivi vikuu vimeonyesha kwa namna moja au nyingine azma ya kupambana na rushwa wakielezea mikakati yao katika mikutano ya kampeni.
Lakini wakati taifa hilo na dunia ina hesabu siku na masaa kabla ya upigaji kura wa Agosti 8, ili kuwapata viongozi wa kitaifa nchini Kenya, kumekuwa na minong’ono mbalimbali vipi vyama hivyo vitaweza kupambana na rushwa iwapo vimeruhusu wafanyabiashara na matajiri kuwachangia.
Maslahi binafsi
Joram Wangira ambaye ni mfuasi wa muungano wa NASA unaounganisha upinzani nchini Kenyaamesema kuwa hakuna ubaya wowote iwapo mgombea atachangiwa fedha.
Lakini ametoa angalizo kwamba ni isiwe kwa ajili ya maslahi binafsi.
“Iwapo atachangiwa fedha kwa sababu ya kushirikiana na matajiri na wafanyabiashara endapo atachaguliwa hapo kuna tatizo,” amesema Wangira.
Akaendelea kusema kuwa mchango huo ni jambo la kawaida kama ilivyo, watu ambao ni marafiki zako kukuchangia pesa kidogo kidogo hakuna tatizo lolote, iwapo tu hakuna hila ndani yake.
Vita ya ufisadi
Frederick Otieno ambaye ni mwanachama wa chama tawala cha Jubilee anasema kuwa kupambana na ufisadi ni jambo linalotegemea msimamo wa kiongozi mwenyewe.
“Mgombea anaweza kuwa nania ya kupambana na ufisadi, lakini pia kuna wale ambao wanataka kuchangisha pesa kwa nia nzuri, hakuna tatizo lolote” amefafanua.
Amesema si kweli kwamba wote wanaochangisha hawataweza kupambana na ufisadi, na kuwa wako ambao wanaweza kupambana na tatizo hilo.
Sasa kama mtu hana uwezo wa fedha lakini ana nia ya kupambana na ufisadi, bado ataweza kusimamia jukumu hilo hata kama atakuwa amechangiwa na wafanyabiashara na matajiri, amesema.
Kitengo cha kupambana na ufisadi
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jubilee Kaunti ya Mombasa, Ali Mwatsahu ameiambia VOA kwamba ndani ya chama cha Jubilee kuna kitengo maalum cha kupambana na ufisadi.
Kamati ya maadili ndio ndiyo inashughulikiamasuala ya ufisadi, na mtu akipatikana na shutuma zozote za kifisadi atatolewa kutoka katika chama.
Amesema kuwa chama cha Jubilee hakina wafadhili na hivyo wanajisimamia wao wenyewe na kuongeza kuwa Jubilee huwa inafanya harambee ili kuchangisha fedha jambo ambalo linakubalika katika chama.
“Pia kunamikakati ya kuwabana viongozi wa Jubilee. Kiongozi akichaguliwa ni lazima afuate ilani ya uchaguzi ya chama,” amesema mwanachama huyo.
Muongozo wa maadili kwa viongozi
Akifafanua mikakati ya NASA katika kupambana na ufisadi, katibu mkuu wa Chama cha Wiper, Hassan Omar ambacho ni mshirika wa NASA,anasema kuna muongozo wa maadili ambao ni namna mpya ya kuweza kukabiliana na ufisadi nchiniKenya.
“Tunasema hakuna mtu yoyote atakayetumika katikanafasi ya serikali ambaye atakubaliwa kufanya biashara na serikali, yeye mwenyewe au kupitia jamaaa zake au watu ambao ana mahusiano nao.
Amesema muongozo wa NASA ni kuwa pale kiongozi anapokutwana shutuma zozote ni mpaka pale mahakama au taasisi ya maadili itakapo mtakasa, hauwezi kuwepo katika wadhifa wake na ni lazima ajiuzulu, ili apishe uchunguzi ufanyike.
Katiba na maadili ya uongozi
Wakili wa Mahakama Kuu mjini Nairobi, David Njoroge amefafanua kuwa katiba iliyopitishwa 2010 ina kipengele ambacho kinazingatia masuala ya maadili ya uongozi.
Anasema mtu yoyote akiingia katika uongozi ni lazima apimwe na sifa ya kuwa mwaminifu na mwadilifu. Pia ni lazima ithibitishwe kwamba hana ufisadi wa aina yoyote na hajihusishi na vitendo vyovyote ambayo ni kinyume cha sheria.
“Sasa kuna mtindo umejitokeza kwamba wanasiasa wanaweza kuwakusanya wafanya biashara na marafiki na washirika wao katika kuchangia harambee zao,” amesema wakili huyo.
Lakini sheria ya vyama vya siasa ambayo ilipitishwa baada ya katiba ya Kenya kupitishwa inazingatia kwamba kuna tofauti kati ya kuendesha vyama vya siasa kwa kutumia pesa za umma na kuendesha kampeni za uchaguzi.
Matarajio ya kulipwa fadhila
Lakini kama tunavyofahamu iko dhana kwamba mwanadamu anapokuchangia anakuwa na matarajio ya kulipwa fadhila. Ana matarajio kwamba baada ya ushindi wa mgombea anaweza kupata manufaa fulani kutoka kwa mgombea huyo.
Wanasiasa wotewanakubaliana kuwa wananchi ndio chachu ya kuwafanya viongozi wawajibike. Ni lazima wao watoe shinikizo kwa viongozi ili waweze kuwajibika.
Kadhalika suala la kupambana na rushwa wadau wote wanakubaliana kuwa matajiri na wafanyabiashara kuwachangia wanasiasa na iwapo halitowaathiri wanasiasa katika kupambana na ufisadi ni jambo ambalo linahitaji mjadala zaidi.
Lakini kila mtu anasubiri kuona iwapo baada ya uchaguzi vyama hivyo vitaweza kutimiza ahadi zao.
Your browser doesn’t support HTML5