Jeshi la Sudan limesema Jumapili kamanda kutoka kwa hasimu wake wa kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) ameondolewa na baadhi ya wanajeshi wake, katika kile ambacho kitakuwa ni hatua ya kwanza ya aina hiyo kufanywa na kiongozi wa ngazi ya juu tangu pande hizo zianze mapigano zaidi ya miezi 18 iliyopita.
Hakuna tamko la haraka kutoka kwa RSF kundi ambalo limechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya nchi katika mgogoro na jeshi ambapo Umoja wa Mataifa unasema umesababisha moja ya mgogoro mbaya zaidi wa kibinadamu duniani. Wafuasi wa jeshi hilo walituma picha mtandaoni wakimuonyesha Abuagla Keikal, afisa wa zamani wa jeshi ambaye alikuwa kamanda wa juu wa RSF katika
jimbo la kusini mashariki la El Gezira, baada ya kuondoka katika kundi hilo. Jeshi ambalo hivi karibuni limeripoti mafanikio dhidi ya RSF katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu, limesema Keikal ameamua kuchukua hatua hiyo kutokana na ajenda zake za zamani za kikosi hicho kuharibika.
Haikuelezea kwa kina na hakuna taarifa iliyotolewa, iliyochapishwa au kwenye video kutoka kwa Keikal.