Jopo la Baraza la Wawakilishi la Marekani lamshutumu Trump kwa uchochezi na uvamizi

Your browser doesn’t support HTML5

Hatimaye uchunguzi wa uliodumu kwa mwaka mmoja na nusu umemalizika na Jopo la Baraza la Wawakilishi la Marekani limepeleka mapendekezo yake Wizara ya Sheria kumfungulia Rais wa zamani Donald Trump mashtaka.

Ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani, jopo la Baraza la Wawakilishi – wademokrat 7 na Warepublikan wawili wanaompinga Trump - kwa kauli moja wamewataka waendesha mashtaka kumfungulia kesi ya makosa manne dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Marekani.

Kamati hiyo ilimtuhumu Trump, ambaye aliondoka madarakani mwezi Januari 2021, kwa kuchochea au kusaidia uvamizi, kuzuia mchakato rasmi wa Bunge wakati lilipokutana kurasmisha ushindi wa Biden, njama ya kuihujumu Marekani na hujuma ya kutoa taarifa za uongo.