Jeshi la Sudan, lajitoa katika mazungumzo ya kusimamisha mapigano

Jeshi la Sudan, Jumatano limejitoa katika,mazungumzo na vikosi vya akiba vya RSF ya kuongeza muda wa makubaliano ya kuendeleza sitisho la mapigano likishutumu kukiukwa kwa mpango wa amani wa Saudi Arabia na Marekani.

Pande zote mbili za mgogoro wa wiki sita zilitia saini kusitisha mapigano kwa siku saba katika mji wa Saudi Arabia wa Jeddah, Mei 20 ikiwa na lengo la kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

Ilipendekezwa kuongezwa muda kwa siku tano kulikubaliwa Mei 29.

Marekani na Saudi Arabia zinaangalia utekelezaji wa sitisho la mapigano, na kusema pande zote zimeyakiuka.

Wakati huohuo baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana Jumatano kwa dakika 90 katika mkutano wa faragha baada ya kuitishwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres. Ni mara tano tu katika kipindi chake cha miaka mitano madarakani ameitisha mkutano kama huo.