Jeshi la Nigeria lauwa waasi 24

Msafara wa jeshi la Nigeria ukiwa na kombora la kutunbua ndege ukielekea Bama, Borno State, Nigeria, August 31, 2016.

Wanajeshi wa Nigeria waliwaua watu 24 wanaoshukiwa kuwa waasi katika mashambulizi mawili kaskazini mashariki mwa nchi hiyo  

Wanajeshi wa Nigeria waliwaua watu 24 wanaoshukiwa kuwa waasi katika mashambulizi mawili kaskazini mashariki mwa nchi hiyo na kuchukua silaha zao , jeshi limesema leo Jumanne.

Boko Haram na tawi lake la Islamic state la Magharibi mwa Afrika (ISWAP) wamekuwa wakipambana na vikosi vya jeshi vya Nigeria kwa zaidi ya muongo mmoja katika mzozo ambao umeua maelfu na kusababisha mamilioni kukimbia makazi yao.

Meja Jenerali Christopher Musa, kamanda wa kikosi cha kupambana na uasi, aliambia Reuters kwamba wanajeshi waliwaua waasi 16 wa Boko Haram kilomita chache kutoka mji wa Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno.

Musa alisema kuwa wakati wa mapambano hayo na waasi malori mawili ya bunduki yalikamatwa na moja likaharibiwa.

Rais Muhammadu Buhari amesema vikosi vya usalama vinafanikiwa dhidi ya waasi kaskazini mashariki mwa nchi na pia dhidi ya majambazi wenye silaha ambao wamefanya utekaji nyara kwa kutaka fidia na kuua mamia kaskazini magharibi.