Jeshi la Marekani lilitangaza Jumatano jioni kuwa linasitisha ndege zake zote za Osprey V-22.
Hatua hii imechukuliwa wiki moja baada ya wanajeshi wanane wa Kamandi ya Operesheni Maalum ya Jeshi la Anga kufariki katika ajali kwenye pwani ya Japan.
Jeshi la Anga na Jeshi la Wanamaji lilichukua hatua ya kusitisha mamia ya ndege baada ya uchunguzi wa awali wa ajali ya wiki iliyopita kuashiria kuwa hitilafu ya vifaa - kwamba mtambo ulienda vibaya kwenye ndege - na kuwa sio makosa ya wafanyakazi iliyosababisha vifo. .
Ajali hiyo iliibua maswali mapya kuhusu usalama wa ndege ya Osprey, ambayo imehusika katika ajali nyingi mbaya katika muda wake mfupi wa kuhudumu.
Japan ilisimamisha ndege yake ya Osprey 14 baada ya ajali hiyo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP