Jeshi la Marekani laanza tena kurusha ndege zisizo na rubani na ndege za uchunguzi Niger

Bendera za taifa za Niger na Mali zikiwa mezani wakati wa mkutano wa ECOWAS. Picha na GERARD NARTEY / AFP.

Wiki iliyopita Pentagon ilisema baadhi ya wanajeshi na vifaa vilihamishwa kutoka kwenye kambi ya anga karibu na Niamey, ambao ni mji mkuu wa Niger, hadi mji mwingine huko Agadez. Niamey iko umbali wa kilomita 920 kutoka Agadez.

Jeshi la Marekani limeanza tena kurusha ndege zisizo na rubani na ndege za uchunguzi kutoka katika vituo vya anga nchini Niger zaidi ya mwezi mmoja baada ya mapinduzi kusimamisha kwa muda shughuli zote hizo huko, mkuu wa Jeshi la Anga la Marekani kwa Ulaya na Afrika alisema Jumatano.

Tangu mapinduzi ya Julai, wanajeshi 1,100 wa Marekani waliotumwa nchini humo wamekaa ndani ya kambi zao za kijeshi. Wiki iliyopita Pentagon ilisema baadhi ya wanajeshi na vifaa vilihamishwa kutoka kwenye kambi ya anga karibu na Niamey, ambao ni mji mkuu wa Niger, hadi mji mwingine huko Agadez. Niamey iko umbali wa kilomita 920 kutoka Agadez.

Akijibu swali kutoka Shirika la Habari la Associated Press juu ya jinsi Marekani iliweza kuendelea na operesheni yake ya kukabiliana na ugaidi bila ndege hizo, Jenerali James Hecker, kamanda mkuu wa Jeshi la Wanaanga Ulaya na Afrika, alisema katika wiki za hivi karibuni kuwa baadhi ya operesheni za ujasusi na ufuatiliaji zimeweza kuanza tena kwa sababu ya mazungumzo ya Marekani na utawala wa kijeshi