Jeshi la Israel limesema siku ya Ijumaa kuwa limewaua makamanda wawili waliohusika katika shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023, likiendeleza mashambulizi yake kaskazini mwa Gaza siku moja baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kutoa hati za kukamatwa kwa vita hivyo.
Huku Israel ikipigana pia na mshirika wa Hamas Hezbollah nchini Lebanon, video za mubashara za AFPTV zilionyesha mashambulizi kadhaa mapema Ijumaa kwenye vitongoji vya kusini mwa Beirut, ambapo kundi linaloungwa mkono na Iran linashikilia mamlaka.
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ilisema siku ya alhamisi kwamba Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa zamani wa Ulinzi Yoav Gallant wanaweza kuwajibika kwa uhalifu wa kivita wa kusababisha njaa kama silaha ya vita na uhalifu mwingine dhidi ya ubinadamu dhidi ya wapalestina na katika eneo la Gaza lililozingirwa.