Jeshi la China lafanya mazoezi zaidi karibu na Taiwan

Mazoezi ya kijeshi ya China. (Hu Shanmin/Xinhua via AP)

Jeshi la China lilisema lilifanya mazoezi zaidi karibu na Taiwan siku ya Jumatatu wakati kundi la wabunge wa Marekani lilipotembelea kisiwa hicho kinachodaiwa ni himaya ya  China na kukutana na Rais Tsai Ing-wen, katika kile Beijing ilisema ni ukiukaji wa uhuru wake.

Wabunge hao watano wa Marekani, wakiongozwa na Seneta Ed Markey, waliwasili Taipei kwa ziara ambayo haikutangazwa siku ya Jumapili, ikiwa ni kundi la pili la ngazi ya juu kuzuru kufuatia ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi mapema Agosti, ambayo ilianza siku kadhaa za Mazoezi ya vita yliyofanywa na China.

Kitengo cha kijeshi cha China kinachohusika na eneo lililo karibu na Taiwan,

the People's Liberation Army's Eastern Theatre Command kilisema kuwa kimepanga doria za pamoja za utayari wa mapigano na mazoezi ya mapambano katika bahari na anga karibu na Taiwan Jumatatu.