Mkasa huo ulitokea katika kijiji cha Kware Pipeline, mtaa wa Embakasi, nje ya mji wa Nairobi.
Kufikia jioni ya Jumanne, takriban watu 15 hawakuwa wanajulikana waliko kufuatia mkasa huo.
Shirika la msalaba mwekundu nchini Kenya, lilisema kupitia ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kuwa makundi ya uokozi yalikuwa kwenye eneo la mkasa.
Mashahidi wameiambia Sauti ya Amerika kwamba magari ya msalaba mwekundu na ambulensi kadhaa zilionekana zikisafirisha watu kutoka eneo la tukio hilo.
Halmashauri ya kupambana na majanga ilisema Jumanne kwamba baadhi ya wakazi walikuwa wametoroka baada ya kuonywa kwamba jengo hilo lilikuwa kwenye hatari ya kuporomoka.
Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, takriban watu 49 walikufa baada ya jengo jingine kuporomoka mjini Nairobi.
Habai zaidi zitafuata.