Watu wenye silaha walimpiga risasi jenerali wa jeshi la Nigeria wakati alikuwa akisafiri kwenye gari kwenye barabara kuu kutoka mji mkuu, Abuja, jeshi limesema Ijumaa, katika shambulio la kwanza la bunduki dhidi ya afisa mwandamizi wa jeshi.
Ujambazi wa kutumia silaha na utekaji nyara kwa ajili ya fidia, hasa kaskazini magharibi, umekuwa wa kawaida sana hivi kwamba wengi wanaogopa kusafiri kwa barabara. Kuongezeka kwa ukosefu wa sheria kote nchini kulisababisha wabunge mwezi Aprili kumtaka rais atangaze hali ya hatari.
Meja Jenerali Hassan Ahmed aliuawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia gari lake Alhamisi kando ya barabara ya Lokoja-Abuja, msemaji wa jeshi Brigadier Jenerali Onyema Nwachukwu alisema katika taarifa. Lokoja, kilomita 200 kusini mwa Abuja, ni mji mkuu wa jimbo la Kogi.