Basi hivi sasa kuna mtengeneza filamu mmoja aliyebahatika kutambuliwa na Hollywood na pia kukubalika kwenye jamii.
Mkurugenzi na mwandishi filamu Lena Khan, mara moja unagundua kuwa halingani na wenzake wakurugenzi wa Hollywood. Anasema hiyo ni changamoto kubwa.
"Ni vigumu sana kuwa mtengeneza filamu mwanamke ndani ya Hollywood. Hiyo ndio ukweli wa mambo. Nafikiri wanahisi kana kwamba hauna uwezo wa kutosha au huwezi kusimamia utengenezaji filamu au wala hawatampa nafasi Muislamu. Nafikiri wanaendelea kutafakari kuhusu hilo," amesema Khan.
Khan ni mtoto wa mhamiaji kutoka India. Akiwa bado shuleni, alitafakari kuhusu nyanja mbali mbali kabla kuamua kujitosa kwenye uwanja wa filamu jambo lililosababisha kukosolewa hasa miongoni mwa jamii yake Wasia.
Khan afafanua : "Wakati niliopanza, watu wengi kutoka jamii yangu Asia kusini walihoji ni kwa nini nilichaguwa taaluma hiyo isiyo na maana."
Licha ya hilo Khan hakuvunjika moyo aliendelea kutafuta ufadhili wa filamu yake kwa jina la Tiger Hunter. Khan anasema kuwa mada ya filamu hiyo kimataifa pamoja na muda muafaka wa kutolewa filamu ilisaidia kupata kwa mafanikio.
"Marufuku dhidi ya waislamu kuingia Marekani ilitokea wakati filamu ilikuwa inatolewa. Hiyo haikuwa imepangwa iwe hivyo. Haikuwa hatua nzuri lakini ilifaa sana wakati huo," alieleza Khan.
Filamu ya Tiger Hunter ilifunguwa milango kwake Khan ambaye anasema kuwa ataendelea kufanya utafiti wake ndani ya Hollywood kwa wakati wake ili kuendeleza taaluma ya kuandika na kusimamia utengenezaji filamu.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Harrison Kamu, Washington, DC.