Japan yaipatia Ukraine magari 100 ya kijeshi ahadi iliyotoa mkutano wa G7

g7Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida akiwa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy katika mkutano wa G7, Japan.

Jeshi la Ukraine linatarajiwa kupokea msaada wa magari 100 kutoka vikosi vya ulinzi vya Japan, kufuatia sherehe ya makabidhiano iliyofanyika mjini Tokyo, Mei 24.

Balozi wa Ukarine nchini Japan, Sergiy Korsunsky alihudhuria sherehe hizo katika wizara ya ulinzi ya Japan kupokea magari hayo akisema kuwa mababidhiano ya magari ya kijeshi kwa mara ya kwanza yalikuwa muhimu.

Makabidhiano hayo yamekuja baada ya Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kuahidi misaada zaidi kwa rais wa Ukraine Volodymir Zelenskiy katika Mkutano wa G-7 huko Hiroshima wiki iliyopita.

Msaada huo wa kishida ni pamoja na magari na mgao wa chakula na huduma za matibabu kwa wanajeshi waliojeruhiwa, wizara ya mambo ya nje ya japan ilisema katika Mkutano huo.