Serikali ya Japan inasema majaribio ya Jumatatu ya makobora yaliyofanywa na Korea kaskazini ni tishio kwa amani na usalama wa Japan na kanda nzima.
Wakati dunia nzima ikijaribu kuzuia kusamba kwa virusi vya corona Korea Kaskazini imeanzisha uchokozi kwa kufyetua duru ya pili ya makombora ya masafa ya mbali katika kipindi cha wiki moja hadi leo.
Msemaji wa seikali ya japan Yoshihide Suga amesema hatua hii ya kurudia mara kwa mara kufyetua makombora ni suala tete linaloikumba jumuia ya kimataifa kwa ujumla.
Jeshi la Korea kaskazini limeeleza kwamba jaribio la leo ni duru mpya ya mazowezi yanayosimamiwa na kiongozi wa Korea kaskazini mwenyewe Kim jong Un.