Japan kutoa msaada zaidi wa chanjo ya COVID ya AstraZeneca kwa mataifa ya Asia

Mfano wa chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca ikiwa kwenye moja ya hospitali huko Taiwan, April 12, 2021.

Dozi zaidi ya milioni 11 zilizotolewa kupitia mpango wa usambazaji dawa wa COVAX zitatumwa kwenda Bangladesh, Cambodia, Iran, Laos, Nepal, na Sri Lanka, pamoja na majimbo mbali mbali ya visiwa vya Pacific, alisema waziri wa mambo ya nje wa Japan Toshimitsu Motegi

Japan itatoa misaada ya ziada ya chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca kwa Taiwan na majirani wengine wa Asia wiki hii waziri wa mambo ya nje wa Japan, Toshimitsu Motegi alisema Jumanne.

Japan itasafirisha dozi milioni moja kwa kila nchi kwenda Indonesia, Taiwan na Vietnam siku ya Alhamis, kama sehemu ya makubaliano ya pande mbili na serikali za nchi hizo, Motegi aliwaambia waandishi wa habari.

Dozi zaidi ya milioni 11 zilizotolewa kupitia mpango wa usambazaji dawa wa COVAX zitatumwa kwenda Bangladesh, Cambodia, Iran, Laos, Nepal, na Sri Lanka, pamoja na majimbo mbali mbali ya visiwa vya Pacific, alisema Motegi.

Wizara ya mambo ya nje ya Taiwan, alishukuru kwa msaada huo, hususan katika kipindi hiki kigumu ambapo Japan inasimama yenyewe kwenye vita vya virusi vya Corona. Japan imechangia kiasi cha dozi milioni 3.4 kwa Taiwan.