Jaji mkuu wa Afrika Kusini, Alhamisi amesema hakuna chochote kitakachozuia mashambulizi ya Israel, huko Gaza, ila mashitaka ya Pretoria dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ni muhimu katika kufichua hali mbaya iliyopo.
Kesi ya Afrika Kusini iliwasilishwa mwezi Disemba 2023 inadai mashambulizi ya Israel ya Gaza, yaliyoanzishwa kwa kulipiza kisasi shambulio la Hamas dhidi ya Israel, ilikiuka Mkataba wa Mauaji ya Kimbari ya Umoja wa Mataifa wa 1948.
Israel imekanusha mashitaka hayo.
Katika mahojiano na AFP, Nambitha Dambuza, jaji wa rufaa katika Mahakama ya Juu ya Afrika Kusini, alilaumu kwamba Israel inakabiliwa na vikwazo vichache katika kuendesha vita vyake.
Mwezi uliopita ICJ iliiamuru Israel kuhakikisha upatikanaji usiozuiliwa kwa wachunguzi waliopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa kuchunguza madai ya mauaji ya kimbari.