Jaji Ketanji Brown kuingia rasmi kwenye ofisi ya Mahakama ya Juu

Jaji Ketanji Brown Jackson akimsikiliza Seneta wa Marekani Cory Booker (D-NJ) akizungumza wakati wa vikao vya uthibitisho vya Kamati ya Seneti ya Marekani kuhusu uteuzi wake katika Mahakama ya juu ya Marekani, k Machi 23, 2022. REUTERS/Elizabeth Frantz/Fil

Jaji Ketanji Brown Jackson ataingia kwa mara ya kwanza kwenye ofisi ya Mahakama ya Juu katika hafla fupi ya mahakama siku tatu kabla ya kuanza kwa muhula mpya wa mahakama kuu.

Rais Joe Biden, Makamu wa Rais Kamala Harris na wenzi wao wanatarajiwa Ijumaa kwenye hafla ya sherehe ya Jackson

Ni mwanamke wa kwanza Mweusi kwenye Mahakama ya Juu. Jackson mwenye umri wa miaka 52 atafuata desturi ya kila jaji mpya tangu 1972 na kuketishwa kwa muda katika kiti ambacho hapo awali kilikuwa cha John Marshall. Marshall alihudumu kama jaji mkuu kwa miaka 34 mwanzoni mwa miaka ya 1800.