Uamuzi wa Jaji wa Jimbo Derrick Watson umezuia amri hiyo ya kiutendaji ya Trump isianze kutumika.
Hawaii ni moja ya baadhi ya majimbo nchini Marekani ambayo yanajaribu kuizuia amri hiyo.
Amri hiyo ilikuwa inaamrisha wasafiri kutoka nchi sita zenye Waislamu wengi kutoingia nchini kwa siku 90 na wakimbizi kwa siku 120.
Rais Trump alisema amri hiyo ingewazuia magaidi kutoka nchi hizo wasiingie Marekani, lakini wako wanaolalamika kuwa ni amri ya kibaguzi.
Amri ya kwanza ya rais aliokuwa ameitoa mwisho wa mwezi wa Januari, iliwachanganya watu na kusababisha maandamano ya kupinga amri hiyo na hatimaye ikazuiliwa na jaji wa Seattle.
Amri ya marufuku iliyokuwa imerekebishwa iliitoa Syria katika orodha ya nchi zilizokuwa zimezuiliwa na pia kuto wahusisha na katazo hilo wale wenye hati za ukazi- green card na uraia pacha
Lakini zaidi ya nusu dazeni ya majimbo ya Marekani yameungana ilikuzuia katazo hilo la kusafiri.