Wanachama wa ISSG wajadili ombi la Libya kuondolewa marufuku ya silaha

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry (kulia) na mwenzake wa Russia, Sergei Lavrov wakiongea na wanahabari baada ya mkutano wa ISSG nchini Ujermani, Februari 12, 2016.

Kundi la mataifa 17 wanachama wa kundi la kimataifa linalounga mkono Syria (ISSG) wanakutana Vienna leo Jumanne kubuni njia za kuboresha sitisho la mapigano na kuwapatia misaada ya haraka ya kibinadamu kwa jamii ambazo zimezingirwa. Afisa mwandamizi wa Marekani amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo ni Agosti Mosi kuwa na muundao wa kazi kwa ajili ya kipindi cha mpito wa kisiasa nchini Syria.

Jana kundi mchanganyiko la nchi 20 na taasisi nne za kimataifa wanafikiria maombi ya serikali mpya ya umoja ya Libya kuondolewa marufuku ya Umoja wa Mataifa ya silaha kusudi iweze kuchukua hatua kumaliza vurugu ambazo zimedumu kwa takriban miaka mitano ikiwa ni pamoja na ongezeko la tishio linaloletwa na Islamic State.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry na mwenzake wa Italia ambao ni wenyeviti wa mazungumzo ya Vienna ambayo yanamjumuisha Waziri Mkuu, Fayez al-Saraj wa Government of National Accord (GNA).

Mchambuzi wa kieneo, Amin Saikal ameiambia VOA kuwa Bw Kerry na wenzake wa Ulaya hawataweka nia ya dhati kwa kuondolewa kwa marufuku ya silaha kama hawana imani kuwa hili litapita kwenye baraza la usalama.

Amin Saikal anasema waandamizi wa IS wamesogea na kuingia Libya huku uwepo wa kundi la wanamgambo wa kisunni ukizidi kuongezeka. Wizara ya Ulinzi ya Mareknai kwa mara nyingine imekiri kwamba timu ndogo ndogo za vikosi maalum vya Marekani viko nchini LIbya. Msemaji Peter Cook amesema wanakutana na wanapata hisia nzuri kuwa wanaohusika huko, ikiwemo uwepo wa IS na kiwango cha nguvu yao.