Isreal kuandaa uchaguzi kwa mara ya 4 katika miaka 2 kutokana na mgogoro wa madaraka

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Israel inatarajiwa kuandaa uchaguzi kwa mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili , baada ya vyama vikuu viwili vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa kushindwa kufikia makubaliano kuhusu bajeti ya majimbo kufikia siku ya mwisho ya kufanya hivyo.

Uchaguzi huo utafanyika mwezi March, ikiwa ni miezi 12 baada ya kufanyika uchaguzi uliopita.

Chaguzi mbili zilizopita hazikufanikiwa kuunda serikali moja thabithi na kupelekea uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alifunguliwa mashtaka ya ufisadi na anatarajia kurejea ofisini kwa mara ya sita.

Amekana madai dhidi yake, akiyataja kuwa yaliyochochewa kisiasa.

Bunge la Israel lilivunjwa moja kwa moja, jumanne usiku namna inavyohitajika kisheria baada ya mda wa mwisho wa kupitisha bajeti ya majimbo ya mwaka 2020 kupita.

Hatua za mwisho za kufanya mazungumzo kuepuka uchaguzi huo zilikosa kufanikiwa.