Israel yatia saini mkataba wa kibiashara na UAE

Waziri wa uchumi wa Israel, Orna Barbivai, kushoto na mwenzake wa UAE Abdulla bin Touq Al Marri.

Israel imetia saini mkataba wa biashara huru na Umoja wa falme za kiarabu ikiwa ni nchi ya kwanza ya kiarabu kufanya hivyo kutokana na kuanzishwa upya uhusiano wa kidiplomasia ulIoshawishiwa na Marekani mwaka 2020.

Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Israel, Mohamed Al Khaja amepongeza mkataba huo akieleza ni mafanikio ya kipekee na ya kihistoria. Amesema biashara kati ya nchi hizo mbili zitaleta faida kubwa kwa kuweza kuingia kwenye masoko ya nchi hizo kwa haraka na kupunguza ushuru kwa pande zote, wakati nchi hizo zinafanya kazi pamoja kuimarisha biashara, kubuni nafasi za kazi na kuimarisha ushirikiano.

Kufuatana na takwimu za Israel biashara kati ya Israel na Emirati mwaka jana imefikia dola milioni 900. Na rais wa baraza la pamoja la biashara kati ya Israel na Umoja wa falme za kiarabu, Dorian Barak ametabiri kwamba biashara kati ya mataifa hayo yataongezeka marudufu na kupindukia thamani ya dola bilioni 2 mwaka huu, na kufikia bilioni 5 katika miaka mitano ijayo. Amesema , karibu makampuni elfu moja ya Israel yatakua yamefungua biasharazao huko Umoja wa Falme za kiarabu ifikapo mwishoni mwa mwaka