Israel yashambulia Lebanon

Mashambulizi ya anga ya Israel yalilenga miji mingi ya kusini mwa Lebanon na Bonde la Bekaa, Jumatano, na kuua na kujeruhi watu, huku mkuu mpya wa Hezbollah akionya kwamba vikosi vyake vitapambana na Israeli mpaka itakapo lazimika kuomba amani.

“Tutamlazimisha adui kutaka kusitishwa kwa uchokozi wake,” Naim Kassem, amesema katika hotuba iliyorekodiwa kutoka eneo lisilojulikana.

Amesema kunaweza kuwa na njia ya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja endapo Israel itasimamisha mashambulizi yake.

Katika jimbo la mashariki la Baalbek-Hermel, Gavana Bachir Khodr, amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba mashambulizi 40 ya Israel, yameua watu 38 na kujeruhi 54.

Amesema kazi ya kuondoa vifusi inaendelea katika maeneo mengi.