Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kuwaondowa wanajeshi wa Kikosi cha Amani cha UNIFIL kutoka maeneo ya mapigano huko Lebanon.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, moja wapo ya waungaji mkono wakuu wa Israel, alizungumza na Netanyahu kwa simu Jumapili na kulaani mashambulio hayo ya Israel.
Italia ina zaidi ya wanajeshi elfu moja katika kikosi cha wanajeshi elfu 10 wa UNIFIL, ikifanya kua nchi inayochangia kiwango kikubwa cha watumishi kwa kikosi hicho.
Ufaransa na Uhispania, kila moja zina karibu wanajeshi 700 kila mmoja kwenye kikosi hicho, zimelaani mashambulio hayo ya Israel.
Katika taarifa nyengine waziri wa ulinzi wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jumapili kwamba, wapiganaji wa Hezbollah hawataruhusiwa kurudi tena kwenye vijiji vya kusini mwa Lebanon, ambavyo anasema wamevigeuza kua vituo vya kijeshi chini ya ardhi ambako wamerundika silaha nyingi.
Katika taarifa ya video, Gallant amesema hawatawaruhusu magaidi kurudi kwenye eneo hilo ambalo ni muhimu katika kuhakikisha usalama kwa wakazi wa kaskazini wa Israel.