Israel imesema Jumapili kuwa imepokea orodha ya mateka wanaotarajiwa kuachiliwa na Hamas baadaye katika sikui hiyo huku Marekani ikisema inaamini kuwa Mmarekani mmoja atakuwa miongoni mwa walioachiliwa na wanamgambo hao kutoka Gaza.
Kuachiliwa huko kwa Jumapili itakuwa duru ya tatu ya mateka kuachiliwa huru katika siku ya tatu ya kile kilichopangwa kama sitisho la siku nne katika mapigano kati ya Israeli na Hamas ambalo linatarajiwa kumalizika Jumanne.
Mshauri wa usalama wa taifa wa White House Jake Sullivan alikiambia kituo cha televisheni cha NBC katika kipindi cha Meet the Press kwamba Marekani ina sababu ya kuamini kuwa walau mateka wake mmoja ataachiliwa huru jumapili.
Maafisa wa usalama wa Israeli wanakagua orodha ya mateka ambayo itatolewa na familia za mateka zimearifiwa, serikali ilisema.