Mkuu wa ulinzi wa Israel, Yoav Gallant, Jumatano amesema maendeleo makubwa yamefikiwa katika kuondoa wasiwasi wa Israeli juu ya upatikanaji wa silaha za Marekani kwa taifa hilo la Kiyahudi.
“Vikwazo vimeondolewa, na kutatuliwa, ili kuendeleza masuala mbalimbali hasa juu kujenga nguvu na usambazaji wa silaha,” Gallant amesema baada ya kukutana White House na Jake Sullivan, mshauri wa usalama wa taifa wa Rais Joe Biden.
Mapema wiki hii, Gallant alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken na Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin.
Marekani ndiyo muuzaji mkuu wa silaha wa Israel, lakini katika wiki za hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, alilalamika kuhusu kile alichosema kupungua kasi ya uwasilishwaji kwa miezi kadhaa.
Maafisa wa White House wamesema walishtushwa na matamshi ya Netanyahu.