Mlipuko mkubwa ulisikika, na moshi mwingi ulionekana ukitanda juu ya vitongoji vya kusini mwa Beirut, ngome ya wanamgambo wa Hezbollah wanaofadhiliwa na Iran.
Afisa wa Hezbollah alisema majengo kadhaa yaliharibiwa na mamlaka ilisema watu wawili waliuawa.
Ripoti za vyombo vya habari huko Mashariki ya Kati zilimtambulisha kamanda wa Hezbollah kama Fuad Shukr, lakini hatma yake ilikuwa haijajulikana.
Chombo cha habari cha Saudia Al Hadath kiliripoti kwamba Shukr alinusurika. Lakini tovuti ya habari ya Israel Ynet ilinuku chanzo cha usalama cha Israel kikisema, “kuna uwezekano mkubwa afisa huyo wa Hezbollah aliuawa. Ikiwa alikuwa katika jengo hilo, hayuko nasi tena.”