Shambulio la hivi karibuni la kuvuka mpaka limekuja siku chache baada ya shambulio la roketi lililoua watoto 12 katika eneo la Milima ya Golan linalodhibitiwa na Israel, huku kukiwa na wasiwasi wa kimataifa kwamba mapigano kati ya Israel na Hezbollah yanaweza kusababisha mzozo mkubwa zaidi wa kikanda pamoja na vita vya Israel na Hamas huko ukanda wa Gaza.
"Ingawa tumeona harakati nyingi kwenye mpaka wa kaskazini mwa Israeli, tunabaki na wasiwasi juu ya uwezekano wa jambo hili kuongezeka hadi kuwa vita kamili," Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin aliwaambia waandishi wa habari Jumanne wakati wa ziara yake nchini Ufilipino.