Mashambulizi ya anga mashariki mwa Syria, ambayo kuna uwezekano yamefanywa na Israel, yameua wapiganaji 23 wanaoiunga mkono Iran, Jumamosi, waangalizi wa vita wameripoti vifo zaidi vinne kaskazini mwa nchi.
Kundi la uangalizi wa haki za binadamu, limesema wapiganaji 23 wanaoiunga mkono Iran, ikijumuisha raia wa tano wa Syria, wanne kutoka kundi la Lebanon, la Hezbollah, raia sita wa Iraq, na wanane wa Iran waliuwawa katika mashambulizi ya anga tisa karibu na mpaka wa Iraq.
Imesema mashambulizi hayo kuna uwezekano yamefanywa na Israel, baada ya hapo mwanzo kuelezwa kuwa kuna uwezekano yalifanywa na Marekani.
Afisa wa jeshi la Marekani ambaye hakutaka kutambulishwa amesema Marekani, haikufanya mashambulizi yoyote nyakati za usiku. Kundi hilo limesema mashambulizi yalilenga maeneo ya Albu Kamal, na mengine yanayozunguka jimbo la Deir el-Zour.