Israel inasema mashambulizi yake ya anga katika ukanda wa Gaza umefanikiwa kugawa ardhi hiyo ya Palestina kwa sehemu mbili siku ya Jumapili.
Msemaji wa jeshi la Israel, Daniel Hagari, amesema kwamba wanajeshi wa Israel, wamezunguka mji wa Gaza, na sasa ukanda huo umegawaika katika pande mbili za Gaza kaskazini na kusini.
Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, amendelea na ziara ya kanda ya mashariki ya kati, kwa ajili ya kukabiliana na tishio la mgogoro huo kusambaa katika kanda zima.
Waziri Blinken, alikutana na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas katika eneo linalokaliwa na Israel, la ukingo wa magharibi Jumapili.
Pia alifanya ziara ya kushtukiza mjini Baghdad, ambapo alikutana na waziri mkuu wa Iraqi, Mohammed Sia al-Sudani.
Wawaili hao walijadili mgogoro wa Israel, na Hamas, na umuhimu wa kuzuia vita kusambaa ikijumuisha mpaka Iraq.