Vikosi vya Israel, vinavyopambana na Hamas vimesema vimegundua handaki kubwa lisilo la kawaida la saruji na chuma, lililotengenezwa ili kubeba mizigo ya wapiganaji kutoka Gaza hadi mpakani.
Kuangamiza mamia ya kilomita za njia za chini kwa chini ni miongoni mwa malengo ya mashambulizi ya Israel, yaliyoanzishwa baada ya wanamgambo wa Hamas kufanya mauaji na utekaji nyara katika miji yake ya kusini na kambi za jeshi Oktoba 7.
Miongoni mwa maeneo ambayo Hamas, ilifanya utekaji katika shambulio hilo ni kivuko cha mpaka cha Erez kati ya Gaza na Israel.
Mita 100 tu kusini mwa kituo cha upekuzi, kilichofichwa kwenye mchanga, jeshi la Israel, liliwaonyesha waandishi wa habari sehemu ya kutokea ya kile llichosema kuwa mradi wa Hamas.
Hamas haikuwa tayari kujibu maombi ya shirika la habari ka Reuters, kujibu madai ya Israel kuhusu andaki hilo.