Israel yaanza kusitisha mapigano Gaza

Usitishaji mapigano uliokuwa ukitarajiwa kati ya Israel na Hamas umeanza baada ya kucheleweshwa kwa karibu saa tatu wakati Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliposema kuwa hautaanza isipokuwa Hamas itatoa orodha ya mateka watatu waliopangwa kuachiliwa Jumapili.

“Waziri Mkuu aliagiza vikosi vya ulinzi vya Israel, kwamba usitishaji mapigano uliopaswa kuanza kutekelezwa saa 8:30 asubuhi, usingeanza mpaka Israel iwe na orodha ya watu waliotekwa nyara ambao Hamas imeahidi kuwaachilia, ofisi ya Netanyahu, ilisema Jumapili.

Hamas hatimaye ilitoa majina na Israel ikaeleza usitishaji wa mapigano utaanza saa 11:15 asubuhi.

Hamas ilitoa chanzo ya kucheleweshwa kwa mgawanyo wa majina hayo ikieleza kuwa ni sababu za kiufundi na kuongeza katika taarifa yake kuwa ilikuwa ikithibitisha kujitolea kwake kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yalitangazwa wiki iliyopita.