Waziri wa Ulinzi wa Israel, Yoav Gallant anasema jeshi lake linahamisha malengo yake taratibu kutoka Gaza kwenda mpaka wa kaskazini wa Israel na Lebanon, huku Israel na wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran wakifanya mashambulizi mapya ya kuvuka mpaka Jumatano.
Baadaye Jumatano, Rais Joe Biden wa Marekani, na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu walizungumza kwa njia ya simu kuhusu vitisho vinavyoikabili Israel.
Viongozi hao wawili walizungumza kuhusu juhudi za Marekani kuiunga mkono Israel dhidi ya vitisho vyote kutoka Iran, yakiwemo makundi ya kigaidi ya Hamas, Hezbollah, na Wahoudhi, kujumuisha katika uwepo wa kijeshi wa Marekani unaoendelea, taarifa ya White House imesema. Biden pia amesisitiza umuhimu wa kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka.