Rais wa Israel amemkabithi waziri mkuu Benjamin Netanyahu, madaraka ya kuunda serikali baada ya kushinda uchaguzi wa mwezi Novemba.
Rais Isaac Herzog amemwambia Netanyahu mjini Jerusalem kwamba ana mamlaka ya kuunda serikali.
Netanyahu alikuwa waziri mkuu wa Israel kwa muda mrefu zaidi kabla ya kuondolewa madarakani mwaka uliopita.
Herzog amesema kwamba baada ya kufanya mashauriano na viongozi wa chama chake, matokeo ya uchaguzi huo yamedhihirika na kwamba jukumu la kuunda serikali ni la Benjamin Netanyahu.
Herzog amesema kwamba anajua kwamba Netanyahu anakabiliwa na mashtaka ya ufisadi mahakamani lakini matokeo ya uchaguzi yanatoa jukumu Netanyahu kuunda serikali kama waziri mkuu.