Kiongozi huyo ambaye amewahi kuhudumu kwa muda mrefu sana kama waziri mkuu wa nchi hiyo, na anayekabiliwa na tuhuma za ufisadi amekuwa kwenye kampeni kali akikipigia debe chama chake cha Likud.
Uchaguzi wa Jumanne utakuwa wa tano ndani ya kipindi cha miaka mitano. Waziri mkuu wa sasa Yair Lapid alichukua nafasi ya Netanyahu mwaka uliyopita, baada ya muungano wa vyama 8 vya siasa kuunda serikali ya muungano.
Kura ya maoni inaonyesha chama cha Netanyahu cha Likud kikiwa mbele ya kile cha Yesh Atid cha Yair, ingawa hilo silo hakikisho kwamba Netanyahu atapata uongozi.
Vyama vyote viwili vinahitaji kuvishawishi vyama vingine vidogo vya siasa, ili kupata wingi kwenye bunge maarufu kama Knesset, mchakato unachukua muda wa wiki kadhaa.