Mfululizo wa picha hizo za kutisha za dakika 44 tayari zimeonyeshwa katika Umoja wa Mataifa huko New York na Geneva mjini Washington, Berlin, Brussels, Madrid na mji mkuu wa Chile Santiago, na pia mjini Paris kwa waandishi wa habari siku ya Jumanne.
“Tumeonyesha filamu hii katika takriban nchi 30. Tunafikiri ni muhimu kwamba watu wajue kilichotokea Oktoba 7," alisema Hen Feder, msemaji wa ubalozi wa Israel nchini Ufaransa.
Shambulio hilo la kushtukiza lililofanywa na kundi la wanamgambo wa Palestina dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba lilisababisha vifo vya watu 1,400 na wengine 240 kuchukuliwa mateka, katika shambulio baya zaidi dhidi ya Israel tangu kuanzishwa kwake mwaka 1948.