Israel imekiri kummua kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh

Mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Hamas Ismail Haniyeh. Agosti 1, 2024

Israel Katz , Waziri wa ulinzi wa Israel, amekiri kwamba Israel ilimuua aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Hamas Ismail Haniyeh.

Haniye aliuawa mwishoni mwa mwezi July akiwa Iran na kuongeza uhasama kati ya Tehran na Israel katika kanda ambayo imetikiswa na vita vya Israel katika ukanda wa Gaza na Lebanon.

Katz amesema kwamba Israel imewashinda nguvu wanamgambo wa Hamas na Hezbollah, Pamoja na kupindua utawala wa Syria.

Alikuwa akizungumza katika hafla ya kutoa heshima kwa wafanyakazi wa wizara ya ulinzi ya Israel.

Amesema kwamba Israel itaendelea kuharibu miundombinu ya kijeshi ya makundi ya wanamgambo na kuua viongozi wao, namna ilivyowafanyia Haniyeh mjini Tehran, Sinwar akiwa Gaza na Nasrallah akiwa Lebanon.

Kundi la wahouthi la Yemen, linaloungwa mkono na Iran limekuwa likishambulia meli za kubeba mizigo katika Bahari ya sham. Limerusha pia makombora na ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya Israel likisema kwaba linafaya hivyo kwa kuunga mkono wapalestina na kupinga vita vya Israel katika Gaza. Israel imeapa kuangamiza viongozi wa kundi la kihouthi.

Mashambulizi dhidi ya Israel kutokea Yemen

Jeshi la Israel limesema mapema leo Jumanne kwamba limezuia kombora lililofyetuliwa kutoka Yemen.

Kombora hilo limesababisha ving’ora kulia, lakini hakuna uharibifu umeripotiwa baada ya kuzuiliwa kabla ya kuingia Israel.

Waasi wa Houthi walio nchini Yemen wamekuwa wakifyetua makombora kuelekea Israel tangu wanamgambo wa Hamas waliposhambulia Israel Oktoba 7 2023, na kupeleeka vita kuanza katika ukanda wa Gaza.

Israel imekuwa ikijibu mashambulizi ya waasi wa kihouthi kwa kutumua makombora ya angani.

Waziri wa ulinzi Israel Katz, ameonya kwamba viongozi wa Houthi watakabiliwa vilivyo namna wa Hamas walivyokabiliwa, sawa na viongozi wa kundi la wanamgambo la Hezbollah nchini Lebanon ambao wameuawa katika mashambulizi ya Israel.

Wanamgambo wa Hamas, Hezbollah, na Houthi wanaungwa mkono na Iran na makundi hayo yanatambuliwa na Marekani kama makundi ya kigaidi.

Wakati huo huo, Katz amethibitisha kwamba Israel ndio ilihusika na shambulizi la mwezi Agosti mjini Tehran, Iran, lililomuua kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh