Iraq imejenga ukuta kwenye mpaka wake na Syria ili kuzuia wanajihadi wa kundi la Islamic state kujipenyeza, chanzo cha jeshi la Iraq kimesema Jumapili.
Katika hatua ya kwanza ya ujenzi, ukuta wa kilomita darzeni kwa urefu na mita 3.5 kwenda juu ulijengwa katika mkoa wa Ninawi, katika eneo la Sinjar kaskazini magharibi mwa Iraq, afisa mwandamizi ambaye hakutaka jina lake litajwe, ameiambia AFP.
Iraq ambayo inagawa mpaka wa zaidi ya kilomita 600 na Syria, inataka kukomesha kupenya kwa wanamgambo wa Islamic State katika eneo lake, chanzo hicho kimeongeza bila kufafanua ni muda gani ujenzi wa ukuta huo utachukuwa.
Mwaka wa 2018, Iraq ilisema ilianza kujenga ukuta kwenye mpaka na Syria kwa sababu hiyo hiyo.