Iran imewafungulia mashitaka raia wawili wa Ufaransa na Mbelgiji kwa ujasusi na kufanya kazi dhidi ya usalama wa taifa wa nchi hiyo.
Mtandao wa Habari wa Wanafunzi usio rasmi kamili ulimnukuu msemaji wa mahakama Jumanne.
Shirika hilo halikutaja majina ya watatu hao wala kusema ni wapi au lini walishtakiwa.
Waziri wa sheria wa Ubelgiji alisema mwezi uliopita kwamba mfanyakazi wa misaada wa Ubelgiji Olivier Vandecasteele, amehukumiwa kifungo cha miaka 28 gerezani nchini Iran kwa kile alichokiita msururu wa uhalifu wa kutengenezwa.
Vyombo vya habari vya Iran vilirusha video mwezi Oktoba ambapo raia wawili wa Ufaransa walionekana kukiri kufanya ujasusi, huku kukiwa na machafuko ya hivi majuzi ambayo Tehran imewalaumu maadui wa kigeni.
Video hiyo ilizua hasira nchini Ufaransa, ambayo ilisema wafungwa hao walikuwa mateka wa serikali.