Iran yaruhusu wakaguzi wa kimataifa kuangalia maeneo nyeti ya nyuklia

Mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya Atomik (IAEA), Rafael Grossi

Tangazo hilo lilitolewa Septemba 12 baada ya mazungumzo mjini Tehran kati ya Rafael Grossi, mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya Atomiki (IAEA) na Mohammad Eslami, mkuu wa taasisi ya nishati ya Atomic ya Iran

Iran imekubali kuruhusu wakaguzi wa kimataifa kutumia kamera za ufuatiliaji katika maeneo yake nyeti ya nyuklia na kuendelea kuchukua picha katika eneo hilo kuepuka mivutano ya kidiplomasia wiki hii.

Tangazo hilo lilitolewa Septemba 12 baada ya mazungumzo mjini Tehran kati ya Rafael Grossi, mkuu wa idara ya kimataifa ya nishati ya Atomik (IAEA) na Mohammad Eslami, mkuu wa taasisi ya nishati ya Atomic ya Iran.

Mazungumzo hayo yalilenga kupunguza mzozo kati ya Tehran na magharibi, ambayo yanatishia kuongezeka na pia mazungumzo ya kijasusi juu ya kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran. "Tulikubaliana kuhusu kubadilishwa kwa kadi za kumbukumbu za kamera za idara hiyo", Eslami alinukuliwa akisema kwa vyombo vya habari vya Iran.