Iran, Jumatatu imeishutumu Marekani, kwa kuchelewesha mazungumzo ya kurejea katika makubaliano ambayo yatadhibiti mipango ya nyuklia ya Iran ili kuondolewa vikwazo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran, Nasser Kanani, amegusia kile alichokiita kuchelewa kwa mwitikio wa maoni ya Iran, iliyopendekeza katika mpango wake toka wiki iliyopita.
Marekani na Umoja wa Ulaya zimekuwa zikifanya tathimini ya mapendekezo hayo ya Iran.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Ned Price, amewaambia wanahabari Alhamisi kwamba thathimini yao inaendelea.
Marekani ilijitoa katika makubaliano hayo mwaka 2018 baada ya aliyekuwa rais wa Marekani, Donald Trump kusema yanaipendelea zaidi Iran.