Iran: Watu wawili wahukumiwa kunyongwa kwa kuukashifu Uislamu

Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Mahakama ya Iran Jumatatu ilitangaza hukumu ya kunyongwa dhidi ya wanaume wawili ambao walihukumiwa kifo kwa kuukashifu Uislamu.

Tovuti ya mahakama, Mizan News iliwatambulisha watu hao kama Yousef Mehrad na Sadrollah Fazeli Zare.

Ripoti hiyo imesema makosa hayo ya uhalifu yanajumuisha kukashifu Uislamu na Mtume Muhammad, na kwamba walitumia mitandao yao ya kijamii kusambaza chuki dhidi ya Uislamu na kuhamasisha kutomuabudu Mungu.

Mahmoud Amiry Moghaddam, ambaye anaongoza shirika la haki za binadamu lenye makao yake Norway , Iran Human Rights, alisema katika taarifa, “ mamlaka kwa mara nyingine zimedhihirisha tabia yao ya kinyama kwa kuwaua watu wawili kwa kutoa maoni yao.”

Ametoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuchukua hatua madhubuti na mara moja.