Iran imeuzia Russia makombora ya masafa marefu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian alipokutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Ryabkov mjini Tehran.

Iran imeipatia Russia makombora yenye nguvu na ya masafa marefu, hatua inayoimarisha ushirikiano wa kijeshi kati ya nchi hizo mbili zilizowekewa vikwazo na Marekani.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba Iran imetoa karibu makombora 400 idadi kubwa ya hayo kutoka familia ya Fateh 110 ya makombora ya masafa mafupi kama Zolfaghar.

Makombora hayo yana uwezo wa kusafiri umbali wa kati ya kilomita 300 na 700.

Wizara ya ulinzi ya Iran na jeshi la ulinzi la Iran linalosimamia mpango wa makombora ya masafa marefu ya Iran, wamekataa kuzungumzia taarifa hiyo, sawa na wizara ya ulinzi ya Russia.

Usafirishaji wa makombora hayo ulianza mapema mwezi Januari baada ya pande zote kufikia makubaliano mwishoni mwa mwaka uliopita.

Vyanzo vya habari nchini Iran vimesema kwamba makubaliano yalifanyika Tehran na Moscow, kati ya jeshi la na wa usalama wa Iran na Russia